Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa ushindi wa Manchester City katika mchuano wa Derby ulitokana na usaidizi wa mechi za kirafiki katika wiki iliyopita.
City imerudi katika kilele cha ligi kuu England au Premier League wakati magoli ya David Silva, Sergio Aguero na Ilkay Gundogan yakiipatia klabu hiyo pointi tatu katika uwanja wa Etihad.
Kwa upande Mourinho amesema kuwa wenyeji hao walikuwa na faida kutokana na kwamba mechi zake mbili za nyumbani dhidi ya Southampton na Shakhtar Donetsk ambapo timu hiyo ilishinda magoli 12- 1 ilikuwa ni ushindi wa wazi ikilinganishwa na mechi ilizocheza timu yake hivi karibuni.
“Tupo nje ya timu nne za juu, tunaweza kulizungumzia vipi taji? Tung’ang’ane kuliziba pengo kuingia katika nafasi ya nne bora, kisha tutazame tofuati.”amesema Mourinho
Manchester United sasa wapo nyuma kwa pointi 12 nyuma ya Manchester City. ambapo kwasasa wanapambana ili kuweza kuingia katika nne bora.
-
Bailly atajwa kikosi cha Ivory Coast
-
Danny Welbeck azua hofu Emirates Stadium
-
Roberto Soldado na wenziwe waadhibiwa Uturuki