Hamisa Mobeto ameachia video ya wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Tunaendana’, ambao ndani yake anaonekana mcheza kikapu wa Marekani, Josh ambaye amekuwa akitajwa kama mpenzi wake mpya.
Katika video hiyo iliyoongozwa na G Ruck, vipande vingi vinaakisi picha na video ambazo Hamisa alikuwa akiweka kwenye mitandao ya kijamii kuhusu penzi lake jipya.
Hata hivyo, bado video hiyo imeacha maswali kama ni kweli Hamisa ana uhusiano wa kimapenzi na Josh na akaamua kumuweka kwenye video hiyo, au ulikuwa mradi wa video tu na hakuna cha ziada.
Majibu anayo Hamisa mwenyewe na hapana shaka yatafahamika punde. Alienda nchini Marekani kwa ajili ya kufanya kazi za burudani na alishiriki katika matamasha kadhaa akiwa na Christian Bella.