Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti, Ismael Ngaile amewahukumu kifungo cha miaka 20 jela wakazi wawili wa wilaya hiyo mkoani Manyara baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kuingia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, kufanya uhalifu, na kukutwa na kucha za Simba.
Hujumu hiyo imetolewa kwa George Seronera (52), mkazi wa kijijicha Bwitengi na Chori Ally (18), mkazi wa kijiji cha Robanda wilayani serengeti, wamehukumiwa baada ya Hakimu kuridhika na ushahidi uliotolewa na mwendesha mashtaka wa Serikali, mbele ya Mahakama ,Emmanuel Zumba.
Hakimu Ngaile amesema mahakama hiyo imejiridhisha pasiposhaka kuwa watuhumiwa walitenda makosa, waliingia ndani ya Hifadhi bila kibali, waliua Wanyama na walikuwa na silaha, hivyo kwa mujibu wa sheria watatumikia jela mika 20 kila mmoja.
Mtuhumiwa Seronera anadaiwa kukamatwa Agosti 4, mwaka 2017 saa 7:00 mchana eneo la Mtu wa Range ndani ya Hifadhi ya Serengeti akiwa na silaha aina ya kisu kimoja, Nyaya 5 za kunasa Wanyama, kichwa cha Pundamilia chenye thamani ya sh milioni 2.616 na kukamatwa na kucha 8 za Simba zenye thamani ya milioni 10.682, kwa upande wa mtuhumiwa Ally alikamatwa Agosti 2017, ndani ya Hifadhi ya Serengeti, kwa makosa mawili kuingia ndani ya Hifadhi bila kibali na kuua swala mwenye thamani ya sh milioni 1.090, hivyo makosa yote mawili atatumikia kifungo cha miaka 20 jela.
Awali mwendesha Mshtaka wa Serikali, Emmanuel Zumba aliomba Mahakama itoe adhabu kali kwa washtakiwa ili iwe fundisho na onyo kwa wengine, kwani vitendo vya kuingia ndani ya hifadhi na kufanya ujangili vinazidi kuongezeka katika jamii.