Serikali ya Tanzania imesaini mikataba ya mikopo miwili ya Dola140 milioni za Marekani (Sh323.39 bilioni) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) kwa ajili ya kufadhili mradi wa kufua umeme wa Malagarasi mkoani Kigoma.

Mkopo huo umesainiwa leo Jumatano Mei 26, 2021 kati ya katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba na mkurugenzi mkuu wa kanda ya mashariki wa AFDB, Nnenna Nwabufo.

Baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, Tutuba amewaeleza waandishi wa habari kuwa kati ya fedha hizo Dola 120 milioni zinatolewa na AFBD na Dola20 milioni zinatolewa na mfuko ukuaji pamoja wa Afrika kutoka Serikali ya China.

Gomes ampotezea wakala wa Kagere
Kunenge azungumza na wakulima pwani