Rais mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, amewataka wananchi kumchagua Mgombea Urais kupitia CCM Dkt. John Magufuli, ili amalizie miradi ambayo haijakamilika.

Amesema hayo wakati wa mkutano wa kampeni za chama hicho jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa Magufuli amefanya makubwa ikiwemo kujenga barabara za juu kwa kiwango cha lami, na kuwataka wananchi kumchagua Magufuli pamoja na wabunge wa chama hicho.

” Magufuli amelibadilisha jiji la Dar es Salaam, kafanya kazi kubwa sana katupatia wali na kitoweo, hospitali nzuri katufanyia mambo mazuri kwa muda mfupi,” amesema Mwinyi.

” Serikali mpya ni ya CCM, mambo aliyofanya Magufuli ni mengi na macho yenu yameona, na masikio yanasikia kwani ni uongo? kwanini tusimpe miaka mimgine mitano ili atuletee maendeleo” amesema Mwinyi .

Azam FC warudia ya 2010/11
Watu kadhaa wauawa katika maandamano Nigeria