Shirika la Afya Duniani (WHO), limesema watu Bilioni 1.8 kote duniani wako katika hatari ya kuambukizwa virusi vya Corona kutokana na ukosefu wa maji katika kituo kimoja kati ya vinne vya afya kote duniani.

Katika ripoti ya pamoja nabvShirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia watoto UNICEF, WHO imesema kuwa ukosefu wa maji ni jambo linalowaweka katika hatari kubwa wagonjwa na wahudumu wa afya katika vituo kama hivyo.

Utafiti huu umefanywa kutokana na takwimu kutoka nchi 165 duniani.

Takwimu za shirika hilo la afya duniani zinaonyesha kwamba huku idadi ya wahudumu wa afya ikiwa ni chini ya asilimia tatu ya idadi ya jumla ya watu, asilimia 14 ya visa vya maambukizi vinavyoripotiwa duniani ni vya wahudumu hao.

Namungo FC kumtumia Shiza Kichuya
Bilionea Subash Patel afariki dunia

Comments

comments