Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta, amesema mlinda mlango, Aaron Ramsdale, alionesha ujasiri baada ya kuepuka makosa mawili ya kipindi cha kwanza katika ushindi wa bao 1-0 wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Brentford, juzi Jumamosi (Novemba 25).

Kai Havertz aliibuka kidedea kwa bao la ushindi kwa kichwa na kuipeleka Arsenal kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England, lakini Ramsdale, kutokana na kuanza kwake ligi kwa mara ya kwanza tangu Septemba, alikuwa gumzo kwenye mechi hiyo.

Kushushwa kwa Ramsdale kwenye benchi nyuma ya David Raya kumezua mshangao, hata hivyo, alipewa nafasi yake ya kung’ara, lakini nusuru aisababishie matatizo Arsenal kwa makosa yake mawili.

Shuti la Bryan Mbeumo lilimshinda na Declan Rice alikuwa karibu na kuokoa hatari, halafu akaupangua mpira kwenye eneo lake la hatari na kuuweza kuidhibiti.

“Ujasiri. Ana ujasiri mkubwa na haiba kubwa na hilo ndilo tunalohitaji,” alisema Arteta alipozungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo.

“Hii ni soka. Nina furaha sana na timu. Jinsi timu ilivvyocheza kwa bao safi. Tunaendelea.

Arsenal hawakuwa katika ubora wao na sare ingekuwa matokeo ya haki, lakini Havertz aliyetokea benchi, aliamsha shangwe kubwa kwa kufunga bao lake la pili msimu huu.

“Huo ndio uzuri wake. Mambo yakija rahisi, huyathamini. Yeye ni mfano kwetu Sote kufanya kile unachopaswa kufanya unapokuwa na matatizo,” alisema Arteta kuhusu fowadi huyo wa Ujerumani.

Arsenal wana pointi 30 mbele ya Manchester City wenye pointi 29, huku Liverpool wakiwa na pointi 28, ingawa bado kuna safari ndefu, Arteta alisema kushika nafasi ya kwanza ni hisia nzuri, hasa katika mechi yake ya 200 akiinoa klabu hiyo.

“Ninapenda kushinda na tuko juu kwenye jedwali na hapa ndipo tunapopaswa kutaka kuwa. Kwangu pia ilikuwa siku maalum michezo 200 na ninataka kusema asante sana kwa kila mtu anayefanya kazi yangu inafurahisha sana,” alisema Mhispania huyo.

Benchikha kutua na wasaidi wake Simba SC
Abdelhak Benchikha kupitisha panga Simba SC