Msichana mwenye umri wa miaka 17 ameripotiwa kubakwa mara ya pili na wanaume wawili waliomfanyia kitendo hicho awali baada ya polisi wa Magharibi mwa India kujaribu kumtumia kama mtego wa kuwanasa wabakaji hao.

Ripoti kutoka nchini humo zilizotolewa na vyombo vya habari vya kuaminika zimeeleza kuwa msichana huyo alifanyiwa kitendo hicho awali Julai 7 mwaka huu, alipokuwa akitembea majira ya jioni ambapo watu wawili walivamia na kumtishia kumuua kwa kisu kabla ya kumbaka.

Watu hao pia walimuibia vitu alivyokuwa navyo ikiwa ni pamoja na simu yake ya mkononi.

Baada siku kadhaa, wanaume hao walianza kumpigia simu yeye na mama yake wakijaribu kuwalaghai kwa kuwatishia kuwa walirekodi tukio hilo kwenye simu hivyo wanampa nafasi nyingine aifuate simu yake.

Msichana huyo aliyekuwa ameripoti polisi tukio la kwanza, alirudi tena katika kituo cha wanausalama hao na kuwaelezea jinsi anavyolaghaiwa na wabaya wake.

Polisi walimtaka apange kukutana nao kama njia nzuri ya mtego wa kuwanasa na kuwaahidi kitika cha fedha ili kuwavuta zaidi.

Msichana huyo aliukubali mpango wa polisi na kutekeleza kama alivyoelekezwa akiamini yuko katika mikono salama.

Hata hivyo, wakati msichana huyo anaenda kukutana na watu hao polisi walifanya uzembe kwa kushindwa kumfuatilia kwa karibu, kosa lililowapa nafasi mafedhuli wale wawili kumbaka tena.

Baada ya tukio hilo, maafisa hao wa polisi walimtupia lawama msichana huyo wakidai hakufuata maelekezo vizuri na kwamba alikosea jinsi ya kuwasiliana.

Kwa bahati nzuri msako mkali wa polisi uliwezesha kuwakamata wabakaji hao. Maafisa waliopanga mtego huo walisimamishwa kazi.

Chanzo: Daily Mail

Rais Atoa Tamko Juu Ya Tajiri wa ‘Unga’ Aliyetoroka Jela Yenye Ulinzi Mkali
Lowassa kuhamia Ukawa? Viongozi Wa Chadema ‘wanena’