Kaimu Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Kihistoria wa Kombe la Mapinzudi Azam FC Abdhamid Moallin, amesema kikosi chake kimekamilisha maandalizi ya kuivaa Simba SC kwenye mchezo wa Fainali utakaopigwa leo Alhamis (Januari 13), Uwanja wa Aman kisiwani Unguja-Zanzibar kuanzia saa Mbili na Robo Usiku.

Moallin amesema kwa kushirikiana na benchi lake la ufundi wamefanya maandalizi mazuri kwa wachezaji na wanaamini mambo yatakua mazuri baada ya kipyanga cha mwisho kupulizwa.

Kocha huyo Raia wa Marekani mwenye asilini ya Somalia, amesema amewaona wapinzani wao, na anawaheshimu, hivyo kikosi chake kitacheza kwa nidhamu kubwa.

“Utakuwa mchezo wa ushindani, tunaenda kupambana kutafuta matokeo mazuri ili kufikia malengo yetu, Simba ni timu nzuri lakini tunaenda kucheza kwa tahadhari kubwa ili kupata ushindi,” amesema Moallin.

Azam FC ilifika hatua ya Fainali kwa kuwafunga Mabingwa wa michuano hiyo mwaka jana (2021) Young Africans kwa Changamotyo ya Mikwaju ya Penati 9-8, baada ya kutoka sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90.

Ikumbukwe kuwa Azam FC ilikutana na Simba SC Januari Mosi Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu, na matokeo hayakua mazuri kwao baada ya kufungwa mabao 2-1.

Kibwana, Ninja waondoka Young Africans
Pablo atamba kutwaa Mapinduzi Cup 2022