Mwanamuziki wa bongo fleva kutoka Kings music Abdul Kiba, ambaye pia ni mdogo wa mwanamuziki Ali Kiba ameyabwaga ya moyoni kuhusu mwenendo wa maisha ya wasanii kutawaliwa na kutokuwepo kwa maelewano baina yao ‘bifu’ na kusema kuwa hakuna faida.

Abdul Kiba ameweka wazi matamanio yake ya kuona siku moja wasanii wote nchini wanakuwa kitu kimoja kwa kuamua kuziweka tofauti zao pembeni na kuungana kuupambania muziki wa bongo fleva.

“Na ‘wish’ wasanii waweze kuachana na bifu na wawe kitu kimoja na hata Ali Kiba na Diamond pia na ‘wish’ waweze kufanya kazi bila kuwa na tatizo lolote. Walishakutana pamoja mara nyingi na kukaa, shida ni mizizi ambayo ilitengenezwa toka mwanzoni, hata Simba na Yanga wakimaliza mechi huwa wanakuwa pamoja,” amesema Abdul Kiba.

Abdu Kiba ameyazungumza hayo mapema leo machi 11, 2022, alipokuwa kwenye mahojiano maalum na kipindi cha Leo Tena cha CloudsFm.

Gucci kuuza chachacha milioni 1
Diara: Ondoeni shaka, tutatwaa ubingwa