Licha ya kuanza majukumu jijini Mbeya, Kocha Abdul Mingange amesema anasubiri kujua hatma yake ya kuitumikia Klabu ya Mbeya City kwa ajili ya msimu ujao.

Mingange ambaye aliwahi kuzinoa timu kadhaa nchini ikiwamo Mashujaa aliyoipandisha msimu uliopita, anatarajia kupewa kibarua cha kuiongoza City ilishuka daraja msimu ujao wa Championship akisaidiana na Mathias Wandiba.

Kocha huyo na msaidizi wake Wandiba, tayari wapo jijini hapa na jana walikuwa wakiiongoza timu hiyo kwenye michuano ya Mbeya Pre Seasons wakisikilizia mabosi wao kusaini mkataba.

Akizungumza jijini Mbeya Mingange amesema kazi yake ni kufundisha soka, hivyo anayo matumaini kwani hadi kuwasili kwake jijini Mbeya ni wito wa mabosi hao na kwamba yeye yupo tayari kufanya kazi.

“Kwa sababu baadhi ya viongozi hawapo na nimeshapewa maelekezo haina tatizo nasubiri leo Jumapili watakapofika wote kujua itakuaje,” amesema kocha huyo mkongwe na Meja msitaafu.

Mwenyekiti wa Mbeya City, Joseph Mlundi amesema uongozi upo makini kutengeneza mipango ya kimyakimya kuhakikisha wanapoanza msimu, timu hiyo itatesa na kurejea Ligi Kuu.

“Kimsingi tusubiri muda utasema, siyo kwamba tumelala kuna mambo tunayaseti na muda wowote mtaanza kuona, tunahitaji City mpya yenye mzuka,” ametamba kigogo huyo.

Man Utd yafufua matumaini kwa Amrabat
RB Leipzig yaichorea mstari Man City