Abiria mwenye bahati aliyetajwa kwa jina la Alex Simon, raia wa Australia, kwa mara ya kwanza katika maisha yake alijikuta akisafiri na ndege kubwa ya Philippines Airline kama mtu aliyeikodi.

Alex Simon, aliiambia Mail Online kuwa alikuwa akisafiri kutoka Manila nchini Ufilipino kwenda Boracay, na alipokuwa anasubiri katika uwanja wa ndege aliambiwa atakuwa peke yake kwa kuwa hakuna abiria mwingine aliye-book safari hiyo isipokuwa yeye.

ndege 2

“Nilipofika uwanja wa ndege nilisikia tangazo na jina langu likisomwa kupitia spika: ‘Bwana Alexander Simon, tafadhari fahamu kuwa hauna sababu ya kusubiri kwa saa mbili ndege bali utaondoka baada ya nusu saa tu kwakuwa hakuna abiria mwingine’, niliambiwa ni mimi pekee,” alisimulia.

Safari ya Simon haikutofautiana na ile ya matajiri wanaokodi ndege kwa ajili ya safari binafsi ila yeye hakuwa hata na rafiki pembeni.

Muigizaji wa ‘Titanic’ akutana na Papa Francis kwa sababu hii
Chadema wadai wako tayari kuchangisha fedha kuilipa TBC irushe Bunge lote 'Live'

Comments

comments