Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, William Mwampaghale amethibitisha kwa ajali ya ndege Precision Air iliyoanguka Ziwa Victoria majira ya aa 2:35 asubuhi ya leo kabla ya kutua uwanja wa ndege wa Bukoba.
Kamanda Mwampaghale amesema manusula wote wamepelekwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Kagera kwa ajili ya matibabu.
“Ndege ilipata ajali mita 100 kabla ya kutua uwanja wa ndege. Abiria wameokolewa na jitihada zinaendelea,” amesema Kamanda Mwampaghale.
Aidha, amewataka wananchi kupunguza taharuki na kuondoka eneo la tukio ili kuruhusu vyombo husika kuendelea na shughuli za uokozi.
Naye, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi Zabron Muhuma, amesema jeshi linaendelea na uokoaji ili kuhakikisha ndege hiyo inatolewa majini.