Nyambizi ndogo ya Titan ambayo ilipata ajali ilipokuwa katika safari ya kutembelea mabaki ya Meli ya Titanic ilikuwa ikiyumbishwa na mawimbi mara kwa mara wakati ikifanya majaribio.
Kwa mujibu wa msafiri mmoja, Arnie Weissmann ambaye alihojiwa na Mhariri Mkuu wa Travel Weekly, amesema wakia kwenye safari ya chini ya maji ya eneo la OceanGate mwezi Mei, mara kadhaa Nyambizi hiyo ilikuwa ikivutwa nyuma na maji na hivyo kukosa uelekeo na kurudi juu.
Amesema, “dhamira yangu ya mwisho iliyopangwa kabla ya kupiga mbizi ya Juni 18 ilikuwa ni Safari lakini nilighairi kwa sababu ya hali mbaya ya hewa na msukosuko niliouona wakati wa majaribio pia ulinipa hofu.”
Hata hivyo, alisema anashangaa iwapo masuala ya kiufundi pia yamechangia kiasi cha kupelekea maafa ya Nyambizi ya Titan, kwani alimuonya Hamish Harding, mmoja wa watu watano waliofariki kwenye ajali hiyo kuhusu ilivyokuwa ikikabiliwa na mapungufu aliyoyaona.