Kwa mujibu wa Chama cha Umoja wa Ngumi za Kiafrika (ABU), chini ya Rais wake, Houchi Houcine kimeweka bayana katika viwango vipya vilivyotolewa kwa mwezi Novemba kuwa Tanzania haina bingwa yeyote wa mkanda huo huku bingwa wa mwisho akiwa ni Tony Rashid aliyeupoteza kwa Sabelo Ngabiyana wa Afrika Kusini.
Tony ambaye amedumu katika nafasi ya Tanzania One kwa kipindi cha mwaka moja kabla ya kung’olewa na Fadhili Majiha anayeshikilia nafasi hiyo huku Tony akiwa katika namba nafasi ya pili ya P4P ya Tanzania.
Orodha ya viwango hivyo ambayo imetolewa na rais wa chama hicho, inaonyesha kwa sasa Tony Rashid amekuwa mshindani ‘Contenders’ kama walivyokuwa mabondia wengine wa Tanzania katika orodha hiyo kutokana na kilo wanazochezea.
Bondia wa Tanzania ambao wemepenya kwenye baadhi ya kilo kama washindani ni Pius Mpenda (Middle) Idd Pialali (Walter), Twaha Kiduku na Dullah Mbabe (Super Middle), Salim Mtango (Super Light), George Bonabucha, Haidari Mchanjo, Ibrahim Mafia, Goodluck Mrema na Innocent Evarist (Bantam), Yohana Mchanja, Muhsini Kizota (Fly).
Katika uzani wa Super Bantam washindani kutoka Tanzania Tony Rashid, Adam Mbega, Hassan Ndonga wakari Light Fly akiwa ni Ally Ngwando huku Super Fly akiwa ni James Kibazange Kwa upande wa uzani wa Feather yupo Nasibu Ramadhan peke yake huku Super Feather wakiwa ni Ibrahim Class na Loren Japhet.