Klabu ya AC Milan imewasilisha ofa mpya yenye thamani ya zaidi ya Euro milioni 20 kwa mshambuliaji wa Chelsea, Christian Pulisic, kwa mujibu wa ESPN.
ESPN iliripoti wiki iliyopita kwamba Pulisic alikubaliana nao maslahi binafsi na Milan, ambapo nyota huyo wa Marekani anataka kucheza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Vyanzo viliiambia ESPN kwamba, Milan wana uhakika wa kufikia makubaliano na Chelsea juu ya ada ya uhamisho, huku klabu hiyo ya Italia ikiamini kwamba akiba ambayo Chelsea ingeweka kwenye mshahara wa Pulisic kama euro milioni 15 kwa mwaka inatosha kupata makubaliano ya ofa yao mpya.
Klabu ya Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1, Lyon pia imeonesha nia ya kutaka kumsajili Pulisic.
Lakini mshambuliaji huyo alikataa ofa kutoka klabu hiyo, akiamini kuwa ni hatua mbaya katika maisha yake ya soka.
Pulisic alijiunga na Chelsea kwa uhamisho wa euro milioni 64 kutoka Borussia Dortmund mwaka 2018 na amefanikiwa kucheza mechi 145 katika misimu minne katika klabu hiyo.