Baada ya mshambuliaji kutoka nchini Colombia, Carlos Bacca kuweka hadharani mipango ya kuelekea msimu mpya wa ligi huko barani Ulaya, uongozi wa klabu ya AC Milan, umevunja ukimya na kukiri wazi wamekubali kumsajili mpachika mabao huyo wa klabu Sevilla.

AC Milan, wamekubali kutoa ada ya Euro milioni 30 kwa ajili ya kusamjili mshambuliaji huyo ambaye atatua San Siro siku kadhaa zijazo kutokana na msimamo ulioonyeshwa na viongozi wa klabu ya Sevilla ya nchini Hispania.

Magwiji hao wa klabu nchini Italia wamefikia hatua ya kukubali kulipa ada hiyo baada ya kushindwa kumnasa mshambuliaji kutoka nchini Colombia, Jackson Martinez, ambaye tayari ameshajiunga na Atletico Madrid akitokea FC Porto ya nchini Ureno.

AC Milan, wamelikua wamejiwekea kipaumbele cha kumsajili Martinez kwanza na kama wangeshindwa kufanya hivyo ndipo wangesogeza kwa Bacca, hali ambayo imekuwa kweli.

Bacca, tayari ameshafikia makubaliano ya kimaslahi na viongozi wa klabu ya AC Milan na imeelezwa kwamba atakua akilipwa mshahara wa paund elfu 50 kwa juma na atasaini mkataba wa miaka minne kuitumikia The Rossoneri baada ya kufanyiwa vipimo vya afya.

Video Mpya: Love Boat - Kcee feat. Diamond Platnumz
AC Milan Wakamilisha Usajili Wa Mfumania Nyavu Kutoka Brazil