Mara nyingi huwa sio kitu kigeni kwa mtu ambaye ni mjasiriamli wakati mwingine kufanya maamuzi yasiyo sahihi, kukosea hapa na pale na hata wakati mwingine kufanya biashara na watu ambao sio sahihi ambao wanauwezo wa kukurudisha nyuma, hii huwa inatokea sana bila kujua.
Unashauriwa kutojihusisha na kila biashara
Ni muhimu kuzingatia na kuweka nguvu zako zote hasa kwenye biashara yako hususani katika kipindi ambacho biashara yako haijakuwa sawasawa. Katika kipindi ambacho unaendeleza biashara yako ili ikue na kufikia viwangi vya juu unavyotaka acha kupenda kujihusisha na biashara nyingine ambazo zinaweza kukupunguzia nguvu kwenye biashara kubwa.
Usitegemee chanzo kimoja cha fedha
Kama una lengo la kuwa mjasiriamali mkubwa katika maisha yako na hatimaye kuwa huru kifedha, acha kutegemea chanzo kimoja cha fedha. Kama utafanya biashara kwa kutegemea chanzo kimoja cha pesa elewa kabisa hutafika mbali sana kimafanikio kama unavyofikiri. Unapokuwa na vitega uchumi vingi hivi vitakusaidia kuongeza pato lako siku hadi siku na utajikuta mwisho wa siku una kiasi kikubwa cha pesa ulichokikusanya kwa matumizi ya leo na baadae.
Acha kuwa na matumizi makubwa ya pesa
Ni hatari sana kutaka kukua kibiashara huku ukiwa ni mtu wa matumizi makubwa ya pesa zako.