Katika hali ya kushangaza, imebainika kuwa Beki wa Kulia kutoka Morocco na Klabu Bingwa nchini Ufaransa Paris Saint-Germain Achraf Hakimi hamiliki chochote, licha ya kulipwa fedha nyingi kama mshahara wake kwa mwezi.

Siri hiyo imebainika baada ya mchezaji huyo kufikishwa mahakamani na aliyekuwa mke wake Hiba Abouk aliyeachana naye Machi 27, 2023 ambapo alikuwa akitaka apewe nusu ya mali za aliyekuwa mumewe.

Taarifa kutoka nchini Ufaransa zimeeleza kuwa, baada ya Mahakama kufanya tathimini za Mali za Achraf ilibaini kuwa aliyekuwa mume wake  hamiliki chochote kwani mali yake yote imesajiliwa kwa majina ya mamake.

Hakimi anapokea Euro Milioni Moja (zaidi ya Shilingi Bilioni 2.56  kama Mshahara ndani ya PSG kila mwezi lakini 80% (zaidi ya Shilingi Bilioni 1.64) pesa hizo huwekwa kwenye akaunti ya mama yake Bi. Fatima.

“Hana mali, magari, nyumba, vito au hata nguo kwa jina lake.Wakati wowote na akitaka chochote huwa anaulizia kwa mama yake ambaye huwa anamnunulia” Mahakama ilitoa taarifa hiyo.

Inakadiriwa Kuwa Hakimi Achraf ana Utajiri wa Euro Milioni 17 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 45 ila Mali zote zinamilikiwa na Mama yake Bi Fatima.

Kichapo cha Man City kimeonesha panapovuja
Naibu Waziri Mkuu wa Slovenia awasili nchini kikazi