Mbunge wa Jimbo la Konde kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Khatib Said Haji amesema masuala ya Tanzania yatazungumzwa Tanzania na sio nje ya nchi hivyo chama hicho hakitakwenda Ujerumani wala Canada kulalamikia masuala ya Tanzania.
Haji ameyasema hayo katia hafla ya uapisho wa Wabunge wanne wa Zanzibar ambapo pia ametoa shukrani kwa Rais Hussein Mwinyi na Maalim Seif Hamad kwa kufikia maridhiano.
Amesema maamuzi yaliyofanywa na Viongozi wa Juu wa Chama cha ACT-Wazalendo yalikuwa ni kwa maslahi mapana ya Wazanzibari na wale wanaokebehi mapatano yao wataona aibu kwa kebehi zao.
Aidha, Haji ameongeza kuwa maridhiano yanapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania badala ya kudharau mapatano hayo na kwamba mambo ya Zanzibar yanahusisha Watanzania hivyo wamesamehe yote yaliyotokea ila watayakumbuka ili yasijirudie tena.