Kamati Kuu ya Chama cha ACT- Wazalendo imeridhia chama hicho kushiriki kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK)   na kuruhusu wawakilishi wa chama hicho  kushiriki kwenye vyombo walivyoshinda.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Desemba 6, jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu  amesema kuwa si kwamba wamefurahia kuchukua maamuzi hayo bali , kamati kuu ya chama hicho ilikuwa ilikuwa njia panda  kimaamuzi.

“Kamati kuu imeridhia kwamba, wawakilishi wa chama waliotangazwa kushinda katika uchaguzi mkuu uliomalizika hivi karibuni, wakashiriki katika vyombo vya uwakilishi ili kuendeleza mapambano ya kudai haki,” amesema Shaibu.

Aidha shaibu ameeleza hatua ambazo zitachukuliwa na chama cha ACT baada ya kukubali kushiriki katika serikali ya Umoja wa kitaifa .

“Kamati kuu ya chama chetu imeielekeza kamati ya uongozi ya chama  kupendekeza jina la mwananchama atakaekuwa makamu wa kwanza wa rais katika serikali ya mapinduzi zanziba”.

Katika hatua nyingine baada   ya kusambaa taarifa kuwa aliyekuwa Mgombea Urais wa hicho  Benard Membe atajitoa katika chama hicho ifikapo Januari 1, 2021. Uongozi wa chama hicho umesema hauko tayari kuzungumzia suala hilo kwa sasa.

Raia wa Ghana kuanza kupiga kura kesho
Waziri Mkuu ahimiza utafiti kilimo cha mboga na matunda

Comments

comments