Chama cha ACT- Wazalendo mkoa wa Njombe kimewaonya viongozi wake wa Majimbo, Vijiji, Wilaya na Mkoa kuepukana na tamaa ya fedha ambazo zinaweza kuwafanya kukitelekeza chama hicho kutokana na hali ya Siasa Ilivyo.

Chama hicho kimejizolea umaarufu mkubwa siku chache zilizopita baada ya aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kutangaza kuhamia katika chama hicho baada ya Mahakama kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa chama hicho.

Akizungumza wakati akiwatambulisha viongozi wa chama hicho ambao wameziba nafasi zilizokuwa wazi akiwemo Katibu wa Mkoa wa Njombe, Kaimu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa, Ally Mhagama amesema kuwa sakata la Maalim Seif Limesababisha wanachama wengi kujiunga katika chama hicho na hivyo umaarufu huo usije wafanya viongozi Kununulika kirahisi.

“Baada ya teuzi hizi watapata ushawishi mwingi sana kutoka chama cha mapinduzi niwaombe sana muwe wavumilivu maana wenzetu wanataka watu ambao wameshatengenezwa na mimi kama mwenyekiti ingekuwa nikufuata pesa ningeondoka mda mrefu kwasababu nimepata ahadi nyingi sana lakini nilikataa kwasababu ya uzalendo kwa nchi yangu,”amesema Ally Mhagama

Kwa upande wake mwenyekiti wa ACT- Wazalendo jimbo la Makambako, Oscar Mgoba Jimbo la Makambako amesema anasikitishwa sana na baadhi ya watu wasiojulikana waliofika katika ofisi yake katika mtaa wa Magegere Mjini humo na Kung’oa Bendera ya Chama hicho.

 

Watendaji sekta ya uchukuzi watakiwa kufanyakazi kwa weledi
Rais akabidhi kitita kwa mchezaji mkongwe wa kandanda timu ya Taifa 'Peter Tino'