Mtangazaji wa kipindi cha XXL cha Clouds FM, Adam Mchomvu amemuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Watanzania kwa ujumla, kwa kitendo cha kumpiga mtama Emmanuel Mbasha kwenye tamasha la ‘Uhuru Kuna Jambo’, lililofanyika jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2020.

Mchomvu alimpiga mtama Mbasha kwa madai kuwa alighafilishwa na kauli aliyoitoa dhidi yake kwenye jukwaa la tamasha hilo lililoandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupambwa na wasanii wengi. Wawili hao walikuwa wakisherehesha sehemu ya tamasha hilo, wote wakiwa wasanii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mchomvu ameandika ujumbe wa kuomba radhi na kueleza kuwa anaendelea kuzingatia maelekezo aliyopewa na jeshi la polisi.

Ameandika:

Dear #WashkajiZangu

Kwanza nimuombe radhi Rais wetu wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Pili kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuniamini na kunipa nafasi ambayo bahati mbaya ilitokea tukapishana kauli jukwaani na bwana ndugu Msanii mwenzangu. Nimepokea simu mbalimbali za Viongozi wa Serikali wakinifahamisha namna nilipaswa kufanya wakati wa shambulio lile la mimi kuitwa ‘ADAM Unajua we ni Bangi sana’ Kwa pamoja nimewaelewa.

Nikutake radhi pia Emmanuel Mbasha Mimi sina tatizo lolote binafsi na Wewe kilichotokea ni kukwazika na kauli yako uliyotoa dhidi yangu kwenye tukio kubwa la Kitaifa lililotazamwa na Mamilion ya Watanzania. Sisi wote Vijana kuna muda tunakosea na tunawekana sawa japo njia zingine si nzuri. Asante kwa Jeshi la Polisi chini ya IGP Simon Sirro kwa maelekezo yenu. Nitayatii na kwa sasa mimi ni Balozi wenu wa hiari kabisa…

Kenya: Mawaziri, makatibu kuchukua likizo ya lazima

Fahamu aina za wateja wa kuwaepuka kwenye biashara

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 17, 2020
Fahamu aina za wateja wa kuwaepuka kwenye biashara