Mpango wa Mshambuliaji wa USGN Victorien Adebayor kujiunga na Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC bado upo njia panda kufuatia Mshambuliaji huyo kufungaka kwa undani juu ya mpango huo.

Adebayor alianza kuhusishwa na mpango wa kujiunga na Simba SC, kufuatia kuonyesha uwezo wake kwenye mchezo wa Mzunguko wa pili wa ‘Kundi D’ Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Mabingwa hao wa Tanzania mjini Niamey-Niger mwezi Februari na timu hizo kufungana 1-1.

Mshambuliaji huyo amezungumza na Dar24 Media na kusema: “Suala la kujiunga na Simba SC siwezi kusema lolote kwa sasa, ni vyema akaulizwa meneja wangu na viongozi wa USGN.”

“Nimesikia mara kadhaa nikihusishwa na mpango huo, lakini kama mchezaji sina budi kuheshimu hilo, kwa sababu ni jambo la kawaida kwa mchezjai kutajwa kwenye mipango ya usajili ya timu nyingine.”

“Sina tatizo mimi kuja kucheza Simba SC, mimi ni mchezaji ninaweza kucheza popote, hivyo kama Meneja wangu na viongozi wa USGN wakikubaliana mimi kuondoka na mambo mengine yakawekwa sawa, nitakuja hapa kucheza.”

Kuhusu Mashabiki wa soka waliomuonyesha upendo na kulitaja jina lake kila wakati akiwa kwenye mchezo dhidi ya Simba SC jana Jumapili (April 03), Adebayor amesema ni jambo jema kwake kuongeza mashabiki kila sehemu anapokwenda.

“Nilisikia jina langu likitajwa tukiwa pale Uwanjani, nimefurahi sana, na sio Uwanjani tu hata tulipokua nje ya Uwanja nilipokutana na watu tofauti waliniita jina langu kwa furaha, kwa kweli nimejisikia furaha sana kuona mashabiki wangu wanaendelea kuongezeka.

Bunge la Tanzania kuanza kurushwa 'Live'
Profesa Mkenda Mwalimu alikuwa mtu wa usawa