Mshambuliaji asiye na timu Emmanuel Adebayor, kwa mara nyingine tena ametupia picha   Instagram kama sehemu ya kuzikukumbusha klabu kuwa yuko tayari kwa usajili wa Januari.

Nyota huyo wa zamani wa Asrenal, Manchester City na Tottenham Hotspur, alikodi mwalimu binafsi mwezi uliopita kuhakikisha kuwa anakuwa fiti vilivyo mwanzo huu wa mwaka 2016.

Aliachwa huru na Totteham mwezi Septemba 2015 baada ya kocha Mauricio Pochettino kuweka wazi kuwa mshambuliaji huyo hayuko kwenye mipango yake.

adebayor

 

Lakini kwa kuwa alikuwepo kwenye orodha ya wachezaji wa Tottenham  kwenye dirisha la kiangazi, hakuwa na uwezo wa kusajiliwa na timu nyingine kabla dirisha lingine la usajili haliwasili.

Adebayor ataingiza jumla ya pauni 5.25 mwishoni wa msimu huu kutoka Tottenham iwapo hatapata timu ya kujiunga nayo.

Gazeti La 'Jambo Leo' latua mikononi mwa Kampuni ya Quality Media Group
Hazard Ahimiza Kuondoka Stamford Bridge

Comments

comments