Mshambuliaji wa kutumainiwa wa USGN ya Niger Victorien Adebayor amekiri kuridhishwa na mazingira ya Tanzania tangu alipowasili akiwa na kikosi cha klabu hiyo kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa Kundi D, Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba SC.

USGN iliwasili Dar es salaam Alhamis (April 31), na kupata muda kujiandaa na mchezo huo, ambao ulipigwa jana Jumapili (April 03), ambapo Simba SC ilishinda mabao 4-0 na kutinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Mshambuliaji huyo amesema kwa kipindi chote alichokaa Dar es salaam- Tanzania amefarijika kuwa na wakati mzuri huku akipata huduma nzuri kutoka kwa Watanzania waliokua karibu na timu yake ya USGN kabla ya kuondoka usiku wa kuamkia leo Jumatatu (April 04).

“Nimependa sana mazingira ya Tanzania kwa wakati wote nikiwa hapa na timu yangu ya USGN, ina watu wakarimu sana, kwa hakika nimependa kila hatua tulikutana nayo hapa, hakukuwa na jambo lolote baya.” amesema Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao 06 kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho msimu huu 2021/22.

Adebayor anahusishwa na mpango wa kusajiliwa Simba SC msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na Michuano ya Kimataifa, kufuatia kuonesha kiwango cha hali ya juu kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Katambi: Ulinzi wa vijana utawezekana kwa kutambua idadi yao
Kilimo Tanzania kuchangia Pato la taifa kwa 10%