Taarifa kutoka nchini Rwanda zinaeleza kuwa klabu ya Simba SC ipo kwenye hatua za mwisho za kumalizana na Kocha wa viungo wa klabu ya APR, Adel Zrane kwa ajili ya kuja kuwa kocha wa viungo wa timu hiyo.
Simba SC hivi karibuni iliwatimua makocha watatu ambo ni Kocha Mkuu, Kocha Msaidizi na Kocha wa Viungo jambo ambalo kwa sasa wanalifanyia kazi kuhakikisha kuwa inawapata makocha hao.
Simba SC wapo katika hatua nzuri za kumshusha kocha Adel Zrane ambaye kwa sasa yupo ndani ya APR akiwa kama kocha wa viungo lakini pia ikiwa kwenye mazungumzo na Kocha Sven Vandenbroeck na Benchikha kwa ajili ya kuja kuwa Kocha Mkuu.
“Simba SC wapo katika hatua nzuri za kumalizana na aliyewahi kuwa kocha wao wa viungo Adel Zrane ambaye kwa sasa ni kocha wa viungo wa timu ya APR ya Rwanda, hivyo kama ambavyo unafahamu wanatakiwa kuvunja mkataba ili waweze kumpata na wapo katika hatua nzuri na huenda siku zijazo akatangazwa kama kocha wa viungo wa timu hiyo.”
“Kwa upande wa kocha mkuu Simba SC bado wapo kwenye mazungumzo na kocha Sven Vandenbroeck kwa ajili ya kuja kuwa kocha mkuu lakini pia wapo kwenye mazungumzo na aliyekuwa kocha wa USM Alger, Abdelhak Benchikha hivyo mmoja wapo kama mambo yatakwenda sawa basi anaweza akapewa timu,” Kimesema chanzo hiko
Kwa upande wa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmedy Ally amesema kuwa: “Simba SC tayari tupo kwenye hatua nzuri za kumtambulisha kocha wetu mkuu, ni bonge la kocha mwenye CV za kushiba.