Waziri wa maji wa Maji, Jumaa Aweso ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji katika Kijiji cha Itelefya uliogharimu kiasi cha 348,757,051.47 Wilaya Momba ambao utazinduliwa na Mwenge wa Uhuru mwezi ujao licha ya kuwa tayari unatoa huduma kwa wananchi zaidi ya 2,448.

Akizingumza mbele ya Waziri wa Maji, Diwani wa Itelefya Wilaya ya Momba ameeleza kuwa mradi huo umewanusuru wakina mama wa Itelefya, waliokua wakitembea umbali mrefu kutafuta maji na wakati mwingine kukumba na vifo kutokana na kuliwa na mamba.

Wananchi wa kijiji cha Itelefya wameishukuru Serikali kwa kuwezesha mradi huo kutekelezwa hasa kutokana na wananchi wa kijiji cha Itelefya, adha waliyokuwa wakiipata ikiwa ni pamoja na kuliwa na mamba wakati wakihangaika kutafuta huduma ya maji.

Sitasahau nilivyovuliwa Uwaziri - Kitwanga
Nini kinafanya Mataifa Makubwa kuihitaji sana Afrika?