Mwanafunzi mmoja nchini  Afrika kusini ambae amesomea mswala ya Tehama anayejulikana kwa jina la  Bright Chabota anasakwa na polisi kwa madai ya kudukua Data za serikali katika Sekta ya Afya kisha kujiajiriri Mwenyewe.

Bright Chabota ambaye alisomea kozi ya uhandisi wa tarakilishi (Computer Engineering) ni wa asili ya Zambia ila mama yake ni wa asili ya Zulu nchini Afrika Kusin, Inaarifiwa hakuwahi kwenda kazini ila amekuwa akipokea mshahara kila mwisho wa mwezi.

Vyombo vya habari nchini humo vinaeleza kuwa, Bright amekuwa akipokea mshahara bila kufanya kazi kuanzia mwezi Juni mwaka jana, hata hivyo serikali ya Afrika ya Kusini ilimgundua Chabota baada ya kukosa rekodi za malipo ya kodi kutoka kwake, ikiwemo ada ya bima ya matibabu nchini humo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Zambiani Observer Bright Chabota alikuwa akijilipa Randi 7000 kwa mwezi ambayo ni sawa na Tsh Milioni 1.2.

Aidha,wazazi wa Chabota tayari wameshahojiwa na kudai kuwa mtoto wao aliwaambia kuwa ameshapata kazi na kwamba alikuwa akilipwa Randi elfu saba kila mwisho wa mwezi kuanzia Juni mwaka wa 2018.

 

 

Afya: Fahamu kwanini unapaswa kula parachichi kila siku
Maambukizi ya Ukimwi yapungua nchini

Comments

comments