Mwanamke mmoja wa Virginia Marekani, Drene Keyes (58), amefariki saa kadhaa baada ya kupewa chanjo ya corona.
Mamlaka zinasema hakuna ushahidi kwamba chanjo hiyo ni chanzo cha kifo na wanaendelea kuchunguza.
Ingawa sababu rasmi ya kifo haijajulikana, Kamishna wa Afya wa Serikali, Norman Oliver amesema Keyes hakufa kutokana na athari yoyote ya mzio iliyohusishwa na chanjo.
Akizungumza na kituo cha habari cha NBC, Mkuu wa polisi wa Warsaw, Joan Kent ameeleza kuwa Drene alipokea chanjo yake ya Pfizer kwenye kliniki ambayo iko maili 80 Kaskazini mwa Newport News, huko Warsaw.
Drene alianza kujisikia kuumwa dakika 15 baada ya kupokea chanjo ya corona na kufariki.