Polisi Mkoa wa Mwanza wanachunguza chanzo cha kifo cha Deogratias Meded (42) Mkazi wa Sengerema aliyefariki dunia muda mfupi baada ya kudaiwa kula makande na chai akiwa kwenye Kampeni za Mgombea Ubunge jimbo la Sengerema kwa Ticketi ya CCM Hamisi Tabasamu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Muliro Jumanne amesema kuwa Marehemu alikuwa Meneja wa Kampeni za Mbunge wa jimbo hilo.

Alifariki dunia ghafla akiwa kwenye msafara wa kampeni, baada ya kula makande na chai alianza kulalamika tumbo linamsumbua, hali yake ilianza kubadilika ghafla na akafariki dunia kabla ya kuanza kupewa matibabu”. amesema Kamanda Muliro.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linafanya uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na idara zingine za uchunguzi ili kuweza kubaini hasa nini chanzo cha kifo chake.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 24, 2020
Maandamano yasababisha Mitihani kusimama Nigeria

Comments

comments