Mtu mmoja amepigwa risasi na kufariki dunia nchini Kenya huku wengine 20 wakijeruhiwa vibaya katika maandamano ya kupinga uchaguzi wa marudio wa urais unaofanyika leo nchini humo.

Maandamano hayo ya wafuasi wa kiongozi wa upinzani NASA, Raila Odinga yamefanyika ili kuweza kupinga uchaguzi kwa madai kuwa haki haiwezi kutendeka na kutoa rais halali atakayeiongoza Kenya.

Aidha, muandamanaji huyo amefariki alipokuwa njiani kupelekwa katika hospitali moja iliyopo mjini Kisumu huku wengine watano wakiwa na majeraha makubwa yaliyosababishwa na kupigwa risasi huku hali zao zikiwa mbaya zaidi.

 

Mafuriko yasababisha kufungwa kwa barabara jijini Dar
Claude Puel ataeuliwa kuwa kocha mpya Leicester City