Mabingwa mara nne wa fainali za Afrika, timu ya taifa ya Cameroon wamepata ushindi wao wa kwanza katika fainali za mwaka huu zinazoendelea nchini Gabon dhidi ya Guinea-Bissau.

Mchezo huo wa kundi A ulishuhudia Cameroon wakitanguliwa kufungwa bao na wapinzani wao katika dakika ya 13 kupitia kwa mshambuliaji wa pembeni wa FC Braga Piqueti Djassi Brito Silva.

Cameroon walizinduka katika dakika ya 61 baada ya kiungo wa FC Brussels Sébastien Siani kufunga bao la kusawazisha na beki wa klabu ya Slavia Prague ya Jamuhuri ya Czech Michael Ngadeu-Ngadjui alifunga bao la ushindi dakika ya 79.

Ushindi huo unaiwezesha Cameroon kuongoza msimamo wa kundi A kwa kufikisha point nne na kuziacha Burkina Faso na wenyeji Gabon wakiwa na point mbili huku Guinea Bissau wakiburuza mkia kwa kuwa na point moja.

Hii leo michuano hiyo inaendelea tena kwa michezo ya kundi B, ambapo mishale ya saa moja kamili jioni kwa saa za Afrika mashariki wapinzani kutoka Afrika ya kaskazini Algeria na Tunisia wataonyeshana ubabe, na mishale ya saa nne usiku Senegal watapapatuana na Zimbabwe.

Real Madrid Wagongwa Tena
Video: Walichosema ACT-Wazalendo kuhusu njaa,wasema CCM imepoteza nafasi yake