Timu ya taifa ya Ghana itaingia katika mchezo wa hii leo, ikiwa inajivunia rekodi ya kufanya vizuri dhidi ya Cameroon ambao ni sehemu ya timu zilizotabiriwa kufanya vyema katika fainali za AFCON za mwaka huu.

Rekodi inaonyesha kuwa Ghana na Cameroon walianza kukutana mwaka 1967, na leo itakua ni mara ya kumi na nne (14) kukutana katika historia.

Kwenye michezo hiyo Ghana wameshinda mara tano, wamepoteza mara mbili na wameambulia sare mara sita, huku wakifunga mabao 15, wamefungwa mabao sita.

Hii leo timu hizi zinakutana kwa mara ya tatu katika fainali za Afrika, na Ghana hawajawahi kuifunga Cameroon kwenye michuano hiyo zaidi ya kuambulia sare mara mbili.

Kwa mara ya mwisho vigogo hawa wa soka barani Afrika walikutana katika mchezo wa nusu fainali ya AFCON 2008, Ghana walikuwa wenyeji wa michuano hiyo na walikubali kufungwa bao moja kwa sifuri mbele ya mashabiki wao.

 

Matokeo ya timu hizi tangu zilipoanza kukutana.

AFCON 2008.

Ghana 0–1 Cameroon

 

AFCON 2000, Kundi A

Ghana 1–1 Cameroon

 

Kufuzu kucheza fainali za AFCON 2000, Kundi A

04.10.1998 Cameroon 1–3 Ghana

 

Mchezo wa kimataifa wa kirafiki 1994

30.11.1994 Ghana 1–0 Cameroon

 

Mchezo wa mkondo wa kwanza wa kuwania kufuzu michuano ya Olimpiki 1988

14.11.1987 Cameroon 2–2 Ghana

 

Mchezo wa mkondo wa pili wa kuwania kufuzu michuano ya Olimpiki 1988

04.10.1987 Ghana 0–0 Cameroon

 

Mchezo wa kimataifa wa kirafiki 1982

05.05.1982 Cameroon 0–0 Ghana

 

AFCON 1982, Kundi A

Cameroon 0–0 Ghana

 

Michezo ya Afrika (All-Africa Games) 1978, Kundi B

Ghana 2–1 Cameroon

 

Mchezo wa mkondo wa kwanza wa kuwania kufuzu michuano ya Olimpiki 1972, Kundi B.

Cameroon 0–3 Ghana

 

Mchezo wa mkondo wa pili wa kuwania kufuzu michuano ya Olimpiki 1972, Kundi B.

Ghana 0–0 Cameroon

 

Mchezo wa mkondo wa kwanza wa kuwania kufuzu michuano ya Olimpiki 1968, Kundi C.

Ghana 3–2 Cameroon

 

Mchezo wa mkondo wa pili wa kuwania kufuzu michuano ya Olimpiki 1968, Kundi C.

13.12.1967 Cameroon 1–0 Ghana

Bunge lapitisha muswada wa marekebisho ya sheria
Video: Siri ya rais Magufuli kukutana na marais wa Afrika Mjini Addis Ababa