Mshambuliaji Sadio Mane usiku wa kuamkia hii leo alianza kuonyesha cheche zake kwenye fainali za Afrika (AFCON 2017) zinazoendelea nchini Gabon kwa kufunga bao lake la kwanza wakati wa mchezo wa kundi B, ambapo Senegal walipambana na Tunisia.
Mane alifunga bao la kuongoza kwa timu yake ya Senegal katika dakika ya 10 kwa njia ya mkwaju wa penati, na dakika 20 baadae Kara Mbodji aliongeza bao la pili na la ushindi kwa Simba hao wa Teranga.
Hata hivyo Tunisia walionyesha upinzani wa kweli dhidi ya Senegal katika mchezo huo uliounguma kwenye uwanja wa Franceville, lakini bahati iliendelea kuwa kwa magwiji kutoka ukanda wa maghrabi mwa barani Afrika.
Mchezo mwingine wa kundi B uliochezwa jana, ulishuhudia timu ya taifa ya Algeria ikitoshana nguvu na Zimbabwe kwa kufungana mabao mawili kwa mawili.
Mabao ya Algeria yalifungwa na kiungo mshambuliaji Riyad Mahrez katika dakika ya 12 na 82, na kwa upande wa Zimbabwe Kudakwashe Mahachi na Nyasha Mushekwi walifunga katika dakika ya 17 na 29.
Hii leo michuano hiyo inaendelea tena kwa michezo ya kundi C ambapo:
Ivory Coast Vs Togo (Saa moja jioni)
DR Congo Vs Morocco (Saa nne usiku)