Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, leo Alhamis (Oktoba 12) itafahamu wapinzani wake watatu katika kundi kwenve Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2023) zitakazofanyika mwakani huko Ivory Coast baada ya Droo itakayochezeshwa mjini Abidjan, kuanzia saa 3 usiku.
Kwenye Droo hiyo itakayoongozwa na kusimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Tanzania itakuwa katika Chungu cha Nne pamoja na Guinea Bissau, Msumbiji, Namibia, Angola na Gambia.
Kitendo cha Tanzania kuwekwa Chungu cha Nne katika Chungu cha Nne kinaiweka katika uweze kano wa kupangwa Kundi gumu kutokana na ubora wa vikosi na wachezaji wa timu zilizopo katika Vyungu vitatu tofauti na ambacho Taifa Stars ipo.
Kwa mujibu wa utaratibu uliotolewa na CAF uchezeshaji wa Droo hiyo kutakuwa na makundi sita yatakayoundwa na timu nne, moja kutoka kila Chungu kati ya vinne vitakavyokuwa na timu sita kila kimoja kulingana na nafasi ambayo ipo katika viwango vya ubora.
Chungu cha Kwanza ambacho timu inayoweza kupangwa na Stars kina Ivory Coast, Morocco, Senegal, Tunisia, Algeria na Misri wakati cha pili kina Nigeria, Cameroon, Mali, Burkina Faso, Ghana, na DR Congo.
Timu mwenyeji, Ivory Coat itapangwa Kundi A na hivyo inasubiri nyingine tatu kutoka katika chungu namba mbili, tatu na nne.
Chungu cha tatu kina Afrika Kusini, Cape Verde, Guinea, Zambia, Guinea ya Ikweta na Mauritani.
Mkurugenzi wa ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ Oscar Milambo amesema kuwa Taifa Stars ipo tayari kupangwa na timu yoyote katika fainali hizo na inasubiri kwa hamu kujua itapangwa na nani.
“Tunaisubiri Droo kuona tutapangwa na nani lakini jambo la msingi ni kufanya maandalizi ambayo yatatufanya tuwe tayari kukabiliana na mataifa ambayo yameshajipambanua kuwa ni makubwa kisoka.”