Baada ya timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars’ kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2023), sasa inasubiri kuona itakuwa kundi gani na nani ikipangwa nazo kwa ajili ya mashindano jayo ya Januari 2024.
Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limepanga kuchezesha droo ya makundi ya fainali hizo Oktoba 12, kabla ya kuanza Januari 13, 2024, mjini Abidjan, Ivory Coast.
2019 Tanzania ilikuwa Kundi C, ilimaliza mkiani bila kuvuna pointi yoyote, ilipokuwa pamoja na Algeria, Senegal na Kenya.
Hii ni mara ya tatu kwa Tanzania kushiriki fainali hizo baada ya zile za 1980, 2019, huku ikichagizwa na ubora wa timu za Simba SC na Young Africans kufanya vizuri mashindano ya CAF pamoja na wachezaji wengi kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.
Maandalizi ya viwanja katika fainali hizo yanaendelea vizuri, huku baadhi ldadi ya yake vikianza kutumika kwenye mechi za kirafiki.
Kati ya viwanja sita ambavyo vitatumika katika fainali hizo mwakani, vitatu tayari vimeshatumiká kwenye mechi za majaribio, ambavyo ni Charles Konan Banny uliopo Yamoussoukro na Stade de la Paix, mjini Bouke.
Jumanne iliyopita, Uwanja wa Alassane Outtara, Ebimpe ulichezwa mechi ya Ivory Coast dhidi ya Mali, huku Jumamosi ikichezwa mechi ya kufuzu, wakati Ivory Coast ikiifunga Lesotho kwa bao 1-0, mchezo uliochezwa Uwanja wa Laurent Pokou wa mjini San Pedro.
Laurent Pokou wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 20,000 ni jina la mshambuliaji wa zamani wa Ivory Coast, huku bao la ufunguzi katika uwanja huo mpya likifungwa na kiungo wa Nottingham Forest, Ibrahim Sangare, wakati Ivory Coast ikifunga Lesotho 1-0.
Rais wa Shirikisho la Soka Ivory Coast, Idriss Yacine Diallo alisema wamekuwa wakijitahidi kuweka mazingira sawa ili timu zilizofuzu ziwe na wakati mzuri katilka fainali hizo.
“Matarajio yetu ni kuona viwanja vingine vyote vikiwa katika hali nzuri na kufikia malengo yetu yote ya vigezo ambavyo vinahitajika kwenye kukidhi mashindano na kufanyika,” alisema Diallo.