Fainali ya Mashindano ya Kombe la Mataifa Huru Barani Afrika (AFCON-2019) zitafikia ukiongoni Ijumaa wiki hii kwa kuwakutanisha miamba Algeria na Simba wa Teranga, Senegal.
Algeria walifanikisha kuvuka mstari wa kuingia Fainali baada ya kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Nigeria, Jana, Julai 14, 2019.
Mara ya mwisho Algeria kuichapa Nigeria ni mwaka 1990 katika fainali za mashindano hayo.
Riyad Mahrez aliyefanikisha upatikanaji wa bao la kwanza la Algeria alichaguliwa na jopo la waamuzi kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Algeria itakutana na Senegal baada ya Simba hao wa Teranga kuichapa Tunisia 1-0, katika mchezo ulioshuhudiwa baadaye. Kilio cha Tunisia kilisikika katika dakika ya 100, kupitia fursa ya dakika za nyongeza baada ya timu hizo kukosa mbabe katika dakika 90 za kawaida.
Mchezo huo uliwasisimua mashabiki hasa baada ya timu zote mbili kukosa penati walizozipata ndani ya dakika chache, hali iliyowaacha midomo wazi mashabiki waliofurika katika uwanja wa 30 June jijini Cairo nchini Misri.