Hatimaye Tanzania imepangiwa kundi katika michuano ya Kombe la Mataifa Huru Barani Afrika (AFCON), huku ikiangukia kwenye kundi C na kufanikiwa kumkwepa mwenyeji.
Katika mchakato wa kupanga makundi uliofanyika jana usiku jijini Cairo, katika kundi hilo Tanzania imengwa pamoja na Algeria, Kenya na Senegal.
Upangaji wa makundi ulifanyika kutokana na ‘Ports’ 4 zilizokuwepo, ambapo kila port ilitoa timu moja ili kuzalisha kundi lenye timu nne. Viwango vya FIFA na CAF vikitumiwa kama vigezo vya kupata timu za kila port.
Kila timu iliyokuwa Port1 iliongoza kundi kisha ikaongezewa timu kutoka port 2-4. Tanzania iliyokuwa kwenye Port 4 ilifanikiwa kumkwepa mwenyeji na kujiunga na jirani zake Kenya pamoja na timu za Algeria na Senegal.
Mashindano ya AFCON yanatarajiwa kuanza Juni mwaka huu. Angalia makundi yote hapa:
Kundi A:
Egypt
DR Congo
Uganda
Zimbabwe
Kundi B:
Nigeria
Guinea
Madagascar
Burundi
Kundi C:
Senegal
Algeria
Kenya
Tanzania
Kundi D:
Morocco
Ivory Coast
South Africa
Namibia
Kundi E:
Tunisia
Mali
Mauritania
Angola
Kundi F:
Cameroon
Ghana
Benin
Guinea-Bissau