Raia wa Afghanistan leo wamesali sala ya sikukuu ya Eid al-Adha, baada ya mapigano kati ya vikosi vya serikali na kundi la taliban kusitishwa kwa siku tatu.

Imeelezwa kuwa wengi wanatarajia makubaliano ya kusitisha mapigano hayo itapelekea kuanzishwa mazungumzo ya kutafuta amani na kumaliza miongo miwili ya mapigano, na hii ni mara ya tatu mapigano kusimamishwa rasmi katika takribani miaka 19 ya mapigano.

Watu 17 wameuwawa leo kutokana na mlipuko wa bomu lilotegwa ndani ya gari, masaa machache kabla ya kuanza rasmi kwa usitishwaji huo wa mapigano. Kundi la Taliban limekana kuhusika na tukio hilo.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 1, 2020
Ruksa wafungwa kutembelewa

Comments

comments