Afisa Mkuu wa uchaguzi Georgia, Brad Raffensperger amesema madai ya Mgombea wa kiti cha Urais kupitia Chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump kuwa alipata ushindi wa jimbo hilo katika uchaguzi uliofanywa 2020, ni ya uwongo na kuyataja kama  “makosa yaliyo wazi”.

Matamshi ya Raffensperger yanawadia baada ya  Trump kumshinikiza katika mazungumzo ya simu yaliyovuja kwamba “atafute” kura za kumuwezesha kupata ushindi.

Trump amekosolewa pakubwa huku baadhi wakidai alichofanya ni sawa na kuingilia mchakato wa upigaji kura kinyume na sheria.

Wabunge wa Republican wanahofia kuwa hatua hiyo huenda ikadidimiza juhudi zao za kupata ushindi katika uchaguzi wa maseneta wa jimbo la Georgia unaofanyika leo Jumanne.

Ikiwa Republicans watapata ushindi katika uchaguzi wa kumchagua Seneti huko Georgia kwenye marudio ya uchaguzi, wataendeleza kudhibiti bunge la juu na ikiwa mgombea wao atashindwa, Democrats watachukua udhibiti wa bunge la Seneti pamoja na bunge la wawakilishi.

“Alizungumza sana na muda mwingi sisi tukawa tunamsikiliza, alizungumza kwa simu kwa takriban saa nzima akiwa na timu yake Jumamosi, na mazungumzo hayo yaliyovuja yalitolewa na gazeti la Washington Post siku iliyofuata, lakini nilichotaka kieleweke ni kuwa takwimu alizonazo ni za uwongo” amesema Raffensperger alipozungumza na shirika la habari la ABC.

Mbunge wa Marekani aapa kuingia na bunduki Bungeni
Tatizo la Vitambulisho vya NIDA kuisha mwezi huu