Jeshi la Polisi mkoani Geita linamshikilia afisa Ugavi kitengo cha Manunuzi cha Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Milembe Suleiman kwa tuhuma za kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Polisi wamemkamatwa afisa huyo mara baada ya mkanda wa video kuzagaa katika mitandao ya kijamii iliyodai kuwa amemvisha pete mwanamke mwenzake kitendo ambacho ni kinyume cha sheria za nchi.

Aidha, katika video hiyo ambayo imekuwa gumzo na kuzua mijadala mkubwa katika mitandao ya kijamii, wengi wamemtaka waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchema na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kuchukua hatua stahiki za kisheria.

Katika video hiyo imewaonyesha wanawake hao wakibusu huku wengine waliokuwa katika tafrija hiyo wakishangilia kwa furaha.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kumshikilia mtuhumiwa huyo akisema kitendo hicho ni kinyume cha sheria.

Hata hivyo, kwa upande wa mwajiri wake GGM, umesema kuwa hauwezi kuingilia kitu chochote katika jambo hilo kwakuwa mambo binafsi.

Gordon Reid atinga nusu fainali Tennis ya walemavu
TFF yaahidi kuifanyia kazi hoja ya Zitto