Afisa Ustawi wa Jamii wa Kituo cha Mahabusu ya Watoto kilichopo Kabwe Kata ya Iyela Jijini Mbeya Groria Kibira(38) amekutwa ameuawa kwa kunyongwa na Watu wasiojulikana kwenye nyumba yake ambayo ipo ndani ya eneo la Kituo cha Mahabusu hiyo .

Akizungumza na Dar24Media Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo watu wanne wanashikiliwa na polisi na kufanyiwa mahojiano ili kubaini chanzo cha mauaji.

Aidha watuhumiwa waliokamatwa kwaajili ya mahojiano ni pamoja na Catherine Chacha wifi yake na marehemu (26), Elia Mwakajinga, Banda Mweupe Simkonde (45) na Joseph Chacha mume wa marehemu

Amesema kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na uchunguzi wa mauaji hayo ya Afisa Ustawi wa Jamii wa kituo cha Mahabusu, hata hivyo Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Bukoba Kagera kwa ajili ya maziko.

Mtoto aliyenasa kwenye kisima afariki dunia
Kamati ya kudumu ya bunge viwanda na biashara yaiagiza SIDO