Mwanadiplomasia mwandamizi wa Korea Kaskazini ambaye alikuwa akihudumu kama Kaimu Balozi nchini Kuwait ameikimbia nchi na kuhamia Korea Kusini pamoja na familia yake.

Kwa mujibu wa gazeti la Mail Business, Ryu Hyun-woo aliwasili Korea Kusini Septemba 2019 na kuomba hifadhi, lakini kuwasili kwake kulifichwa hadi sasa.

Karibu Wakorea Kaskazini 30,000 wameikimbia nchi kutokana na mateso na umaskini chini ya utawala wa kikomunisti na kuhamia Korea Kusini, wengi wao wakiingia kwanza kwa njia ya siri kupitia mpaka wa nchi hiyo na China.

Matukio ya maafisa wa ngazi ya juu kuikimbia nchi hiyo ni nadra, ingawa kuwasili kwa Ryu kumetokea miezi miwili tu baada ya aliyekuwa Kaimu Balozi wa Korea Kaskazini nchini Italia, Jo Song Gil kuomba hifadhi Korea Kusini.

Simba SC yamkana Zahera
Nyoni aondoka kambi ya Stars, arejea nyumbani Tanzania