Afisa mtendaji wa tume huru ya uchaguzi nchini Kenya IEBC, Ezra Chiloba, ametangaza kuchukua likizo ya wiki tatu kuanzia sasa hivyo kutohusika katika mchakato wauchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu.

Hayo yamejiri siku mbili tu baada ya mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati, kuwataka maafisa wote waliotuhumiwa kuchangia kwa dosari zilizogubika uchaguzi wa tarehe nane mwezi Agosti kujiuzulu ili kuhakikisha kuwa zoezi la marudio la tarehe 26 litakuwa la haki na ukweli.

Aidha, Chiloba ni mmoja wa maafisa ambao wamekuwa wakishinikizwa kujiuzulu kabla ya muungano wa vyama vya upinzani NASA kukubali kushiriki katika mchakato wa marudio ya uchaguzi.

“Nimeamua kuchukua hatua hii ili kuweza kurejesha imani kwa wadau ambao wamekuwa wakilalamika kuhusu maafisa waandamizi wa tume kwamba ndiyo kiini cha kuvuruga uchguzi, hivyo sitahusika kwa chochote katika uchaguzi huu wa marudio,”amesema Chiloba

Hata hivyo, mgawanyiko mkubwa umejitokeza ndani ya tume huru ya uchaguzi nchini Kenya IEBC siku chache tu kabla ya uchaguzi huo wa marudio kufanyika.

 

Marais wastaafu Marekani wamkosoa Trump
Mesut Ozil kutimkia Manchester United