Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amefunguka kuwa tayari amepata mafaili muhimu ya wapinzani wake Al Ahly kuelekea katika mchezo wa ufunguzi wa mchezo wa African Football League (AFC), unaotarajia kupigwa Oktoba 20, mwaka huu jijini Dar.
Simba SC wana kibarua cha kutafuta matokeo mazuri katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa michuano ya AFL wakiwakaribisha AI Ahly, Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.
Robertinho amesema licha ya kutokamilika kwa wachezaji wote na wengine kwenda kwenye majukumu ya timu za taifa, analazimika kuwa makini kwa walikuwepo kufanya majukumu yao ikiwemo kujifua zaidi dhidi ya AI Ahly.
“Al Ahly ni timu kubwa na imekuwa na uzoefu wa michuano mikubwa pamoja na kuwa na wachezaji bora, lakini anaimani Simba SC nao ni wakubwa na kuweza kupata matokeo mazuri katika mchezo huo.
“Tumekuwa tukifanya kazi mechi baada ya mechi, tulifanya vizuri mechi za ligi na sasa tunasuka kukosi chetu kuelekea mchezo wetu dhidi ya Al Ahly, tunafahamu ubora wa wapinzani wetu lakini pia wana madhaifu yao yote.
“Hata kwetu tumekuwa bora katika kila nafasi lakini tunazidisha umakini safu ya ulinzi kwa kutorudia makosa tuliyoyafanya kwenye mechi za ligi kuruhusu bao pia kutumia nafasi wanazotengeneza kupata ushindi” amesema Robertinbo