Wekundu Wa Msimbazi Simba kesho watacheza mchezo wa pili wa kirafiki dhidi ya African Lyon inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ligu kuu ambayo inatarajia kuendelea baada ya michezo ya kombe la shirikisho.

Mchezo wa Simba na African Lyon utachezwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kuanzia Saa 1:00 usiku.

Katika mchezo huo Simba inatarajiwa kuongezewa nguvu na wachezaji wake waliokuwa kwenye kikosi cha Tanzania, Kilimanjaro Stars kwenye michuano ya CECAFA Challenge.

Mchezo wa kwanza kwa kikosi cha Simba tangu kiliporejea mazoezini siku kadhaa zilizopita, ulikua dhidi ya KMC, ambapo waliibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja.

Siku hiyo, KMC inayofundishwa na kocha na mchezaji wa zamani wa Yanga, Freddy Felix Minziro, ilitangulia kupata bao lililofungwa na Reyman Mgungila dakika ya saa kwa shuti la mpira wa adhabu nje kidogo ya 18, kabla ya Simba kutokea nyuma na kushinda 3-1.

Mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco mawili, moja kwa penalti dakika ya 27, baada ya Mohamed Ibrahim ‘Mo’ kuangushwa ndani ya penati boksi na lingine dakika ya 86, ambalo lilikuwa la tatu baada ya winga Mzambia, Jonas Sakuwaha aliye kwenye majaribio kufunga la pili dakika ya 39.

Video: UN watoa neno kuhusu wanajeshi waliouawa DRC
Haji Mwinyi Ngwali kuikosa The Cranes Kesho