Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amezisihi nchi za Afrika kuandika upya kuhusu bara la Afrika kwa kuelezea simulizi zao wenyewe.
Rais Samia ameyasema hayo katika Mkutano wa Kimataifa wa 23 wa Baraza la Utalii Duniani
– WTTC, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano nchini Rwanda.
Amesema Serikali za Afrika lazima zijitafakari upya ili utalii uweze kushamiri ikiwemo kujitangaza kimkakati, kufanya utafiti na uhifadhi na kwamba katika zama hizi za taarifa potofu, Afrika haitakiwi kukaa kimya na badala yake ieleze ukweli wa bara hilo.
Aidha, Rais Samia amesema iwapo kweli Afrika ikitaka kuendelea kuwa na vivutio vya asili ni lazima itoe kipaumbele kwenye uhifadhi na kuunga mkono jitihada za kutunza maeneo ya kiutamaduni, kazi za sanaa hususan za kihistoria na mila kwa vizazi vijavyo.