Afrika Kusini imekosoa ujumbe wa Rais wa Marekani, Donald Trump aliouandika katika ukurasa wake wa Twitter kwa madai kuwa ni kuchochea chuki baina ya watu wa rangi mbali mbali.

Katika ujumbe aliutoa hivi karibuni, Rais Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa, Wakulima wazumgu wamekuwa wakinyang’anywa mashamba na kuuawa.

Aidha, Trump amesema kuwa amemuagiza Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo kufuatilia kwa karibu yanayojiri Afrika Kusini katika unyang’anyaji na utaifishaji wa ardhi na mashamba na vitendo vya mauaji ya kiwango cha juu cha wakulima wa kizungu.

Ujumbe huo wa Tweet uliotolewa na Trump unaelekea kuwa ni majibu dhidi ya pendekezo la Rais Cyril Ramaphosa juu ya sera ya mageuzi ya ardhi nchini Afrika Kusini.

Hata hivyo, Serikali ya Afrika Kusini imemjibu Trump katika ujumbe kupitia akaunti yao rasmi ikisema kuwa inapingana na uelewa finyu wa Trump ambao unataka kuligawanya taifa hilo kwa kulikumbusha ukoloni.

 

 

Mbowe: Hatuogopi jela, tunataka tufungwe kwa haki
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 24, 2018