Afrika Kusini imetoa kibali cha kukamatwa Nabii na Mchungaji maarufu wa Kikristo, raia wa Malawi Shepherd Bushiri baada ya nabii huyo kukwepa dhamana na kurejea nchini kwao Malawi.

Bushiri anakabiliwa na mashitaka 419 ikiwa ni pamoja na utakatishaji wa fedha nchini Afrika kusini.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Nabii Bushiri na mkewe Nabii Mary Bushiri, waliandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa waliondoka Malawi kwa sababu ya masuala ya kiusalama.

Bosi wa Jamii Forums ahukumiwa kifungo cha nje

Mwezi uliopita maafisa walimkamata Bushiri na mkewe, akituhumiwa kwa makosa ya wizi wa mamilioni ya dola na kuhusika katika sakata la ufisadi ambapo mapema mwezi huu waliwapatia dhamana ambayo ilikuwa na sharti kwamba lazima wasalimishe hati zao za kusafiria kwa mamlaka za Afrika Kusini.

Ingawa mpaka sasa haijulikani jinsi Bushiri alivyoondoka Afrika Kusini, yapo madai kwamba alitoroshwa na msafara wa rais wa Malawi wakati akiondoka Afrika kusini kutokana na urafiki mkubwa uliopo kati ya Bushiru na Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera.

Afrika Kusini yatoa hati ya kukamatwa kwa Mchungaji tajiri zaidi Afrika

Mhubiri huyo, aliyekuwa na dhamana na ambaye alikuwa akingojea kesi akishtakiwa kwa utapeli wa pesa na ulaghai, awali alikuwa amesema anataka kusafisha jina lake.

Nabii Mchungaji Shepherd Bushiri ni mzaliwa wa Malawi ambaye huendesha shughuli zake za “unabii” katika makanisa mbalimbali kuanzia Ghana hadi Afrika Kusini.

Ni muanzilishi wa kanisa la Evangelical Church Gathering for South Africa lenye matawi yake katika nchi nyingine na anasemekana na wengi kuwa ndiye kiongozi wa kidini tajiri zaidi barani Afrika.

Ntibazonkiza: Simba SC walitaka niikache Young Africans
Mwili wa askari aliyedaiwa kuuawa Pemba wapatikana